Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
KAMPUNI YA URUS YAIKABIDHI TALIRI MTUNGI WA KUHIFADHIA MBEGU ZA MALISHO
24 Feb, 2025
KAMPUNI YA URUS YAIKABIDHI TALIRI MTUNGI WA KUHIFADHIA MBEGU ZA MALISHO

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) imepokea mtungi wa kuhifadhia mbegu za mifugo kutoka Kampuni ya URUS Tanzania inayojishughulisha na uingizaji na usambazaji wa mbegu bora za mifugo.

Akiongea wakati akikabidhi mtungi huo Bw. Edson Mfuru Meneja wa Kampuni hiyo Mkoa wa Arusha amesema lengo la kutoa mtungi huo ni kuwezesha shughuli za utafiti wa mifugo nchini, na hivyo kampuni itaendelea kushirikiana na TALIRI katika kuhakikisha malengo ya utafiti yanafikiwa.

Akishukuru baada ya kupokea mtungi huo Mkurugenzi Mkuu wa TALIRI Prof. Erick Komba amesema upatikanaji wa mtungi huo utasaidia kuwezesha shughuli za utafiti wa mifugo hususani matumizi ya mbegu bora za mifugo kwa njia ya uhimilishaji.

Aidha, Prof. Komba ametoa wito kwa wadau wengine kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha shughuli za utafiti wa mifugo zinafanikiwa.