Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
Wanyama Wakubwa Wanaocheua

TALIRI tunafanya utafiti wa wanyama wakubwa wanaocheua kwa lengo la kuboresha mbari kulingana na mazingira ya wafugaji katika kanda saba za kiikolojia za Tanzania. Tafiti mbalimbali zinalenga kutengeneza wanyama chotara wanaohimili mazingira ya joto ya Tanzania kwa kuunganisha mbari za kisasa kutoka  Ulaya na mbari zinazovumilia joto kali kutoka Asia na Amerika Kusini na kisha kuunganisha na mbari za asili ya Afrika hasa Tanzania ambazo zinavumilia magonjwa, joto kali, mazingira magumu, malisho na lishe duni, ukame, ukosefu wa mali, kujilinda na wanyama wakali na hali ya kutembea umbali mrefu.

Licha ya tafiti kuendelea kuboresha wanyama wa asili ili kupata wanyama chotara bora zaidi kwa uzalishaji wa maziwa na nyama, tumeendelea kufanya tafiti na kutoa elimu ya namna ya kufanya ufugaji bora kwa wafugaji wetu. Lengo letu ni kuwatoa kwenye ufugaji wa asili usio na tija na kuwafanya kuwa wafugaji wa kisasa na kibiashara. Tunafanya tafiti na uendelezaji wa masuala la menejimenti za wanyama, miundombinu, uzalishaji malisho, masoko na mnyololo wa thamani na uboreshaji wa usimamizi wa afya za wanyama wakubwa wanaocheua. Kwa sasa tafiti zifuatazo zimekuwa zikifanyika, zinafanyika na zingine zinatarajiwa kufanyika hivi karibuni:

1. Utafiti wa ngómbe wa kisasa wa maziwa ili waweze kuhimili mazingira ya Tanzania. Utafiti huu unajikita kutafta namna bora ya kufuga ngómbe bora kama Friesian, Jersey, Ayrshire, Girlando,Danish Red, Brown Swiss na Simmental

2. Utafiti wa ngómbe wa kisasa wa nyama ili waweze kuhimili mazingira ya Tanzania. Utafiti huu unajikita kutafta namna bora ya kufuga ngómbe bora kama Brahman, Sahiwal, Simmental, Beefmaster, Angus, Hereford,Charolais na Chianina

3. Utafiti wa ngómbe chotara wa maziwa anafaa kufungwa katika kanda ya Pwani. Kwa sasa tunangómbe chotara waliopo katika kituo cha Tanga

4. Utafiti wa ngómbe chotara wa maziwa na nyama anaefaa kufungwa kanda ya kati yenye ukame na mvua chache. Utafiti huo umewezesha kupatikana kwa ngómbe aina ya Mpwapwa

5. Utafiti na uhifadhi wa ng'ombe bora wa nyama wa asili aina ya Ankole, Borani, Singida White, Iringa Red na Ufipa

6. Utafiti wa ng'ombe bora chotara kwa ajili ya nyama kwa kuunganisha ngómbe wa asili na ng'ombe wa kisasa

7. Utafiti wa mbogo maji kwa ajili ya kuzalisha nyama na maziwa katika mazingira ya Tanzania