Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
Wanyama Wengineo

Taasisi inafanya utafiti na kuwaendeleza wanyama wengineo hasa punda, ngamia na farasi. Lengo la kuwahifadhi ni kuwalinda dhidi ya uwezekano wa kutoweka na tunaamini baado ni wanyama muhimu katika jamii ambao wanatumika kama nguvu kazi huku wakitoa maziwa, nyama na samadi. Pia wanyama hawa ni muhimu katika masuala ya kijamii, kitamaduni, kihistoria na kiulinzi. Wanyama hawa pia wanasaidia usafiri kwa wafugaji maeneo ya mashambani ambako hakuna miundombinu mizuri ya usafiri. Katika mazingira ya ukame, uhaba wa malisho na maji na joto kali unaweza kuendelea kupata maziwa bora kabisa kutoka kwa ngamia ambapo pia unaweza kuyauza kwa bei kubwa sana. Nyama ya ngamia inauzwa kwa gharama kubwa sana, hivyo ni fursa nzuri.

Kwa sasa tunaendelea na mradi wa kuhifadhi na kuendeleza punda katika kituo cha TALIRI Kongwa kilichopo Kanda ya kati.