Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
PROF. MUSHI AIPONGEZA TALIRI KWA UGUNDUZI WA TEKNOLOJIA
13 Aug, 2025
PROF. MUSHI AIPONGEZA TALIRI KWA UGUNDUZI WA TEKNOLOJIA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi, Elimu na Teknolojia Prof. Daniel Mushi ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kuibua na kuendeleza teknolojia bora za mifugo zinazowanufaisha wafugaji nchini.

Prof. Mushi ametoa pongezi hizo leo tarehe 06/08/2025 alipotembelea banda la Taasisi hiyo yanapoendela Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ‘Nanenane’ katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Pamoja na pongezi hizo Prof. Mushi ameeleza kufurahishwa na Mradi wa uboreshaji wa kuku wa asili ya kitanzania aina ya Horas unaotekelezwa na taasisi hiyo na ameitaka taasisi hiyo kuweka mikakati ya kusambaza kuku hao kwa wafugaji.

Akiongelea kuku hao Meneja wa Sehemu ya Uhaulishaji wa Teknolojia wa Taasisi hiyo amesema Mradi umepanga kuzalisha kuku mwenye uwezo wa kutaga mayai 200 - 240 kwa mwaka na kufikia uzito wa kilo 1.5 ndani ya wiki 16 huku kuku wengine wa asili wasioboreshwa hufikia uzito wa gramu 1,200 - 1,500 kwa mwaka na kutaga wastani wa mayai kati ya 30 - 45 kwa mwaka.

Katika maonesho hayo TALIRI imejipanga kutoa elimu ya teknolojia bora za mifugo ikiwemo malisho na mbegu za malisho, mbari za mifugo na vyakula vya mifugo