Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
WAFUGAJI WA MUHEZA WAJIFUNZA TEKNOLOJIA YA 'SPRAY RACE' KUMARISHA AFYA YA MIFUGO
25 Feb, 2026
WAFUGAJI WA MUHEZA WAJIFUNZA TEKNOLOJIA YA 'SPRAY RACE' KUMARISHA AFYA YA MIFUGO

Teknolojia ya kisasa ya kuogeshea mifugo kwa mfumo wa ‘spray race’ iliyopo katika shamba la mifugo la ASAR lililopo wilayani Mufindi mkoani Iringa limeendelea kuwa suluhisho muhimu katika kudhibiti kupe na magonjwa ya ngozi kwa ufanisi. Wafugaji wa ng’ombe wa maziwa kutoka wilayani Muheza mkoani Tanga wanaonufaika na Mradi wa Maziwa Faida walipata fursa ya kujifunza matumizi ya teknolojia hiyo wakati wa ziara yao ya mafunzo mkoani Iringa, iliyolenga kuwajengea uwezo katika mbinu bora na za kisasa za ufugaji wa ng’ombe wa maziwa.

Kupitia mfumo huo wa spray race, wafugaji walijifunza namna unavyosaidia kudhibiti magonjwa yaenezwayo na kupe na hivyo kuimarisha afya ya mifugo na kuongeza tija katika uzalishaji wa maziwa.

Ziara hiyo imewezeshwa na Mradi wa Maziwa Faida unaofadhiliwa na Ubalozi wa Ireland Tanzania na kutekelezwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Kanda ya Mashariki kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti na Maendeleo ya Sekta ya Kilimo na Chakula ya nchini Ireland (Teagasc), kwa lengo la kuboresha mnyororo wa thamani wa ng’ombe wa maziwa na kuongeza kipato kwa wafugaji.