KILIMO IKOLOJIA NI NGUZO YA JAMII IMARA NA ENDELEVU, PROF. KOMBA
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Prof. Erick Komba, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika teknolojia na mbinu za kilimo ikolojia zinazoongeza tija ya mazao na mifugo huku zikilinda rasilimali za asili.
Akizungumza katika Kongamano la Ubunifu wa Mandhari na Mifumo ya Mazingira 2026 lililofanyika jijini Dodoma kupitia Mradi wa Kujenga Jamii Imara na Zenye Ustawi Kupitia Mbinu Shirikishi za Kilimo Ikolijia katika Maeneo Kame ya Tanzania (RESCOMM) Prof. Komba amesema ushirikiano kati ya taasisi za utafiti, serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo ni muhimu katika kusambaza teknolojia zilizothibitishwa kuleta matokeo chanya kwa wakulima na wafugaji.
“Kilimo ikolojia si tu njia ya kuongeza uzalishaji, bali ni msingi wa kujenga jamii imara, zinazostahimili mabadiliko ya tabianchi na kuhifadhi mazingira kwa vizazi vijavyo.” Ameeleza Prof. Komba.
