WIZARA YAMIFUGO YAANZA UTEKELEZAJI WA BBT PROJECT 1 TALIRI KONGWA
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza kutekeleza Mradi wa BBT Project I wa miaka mitano katika Kituo cha TALIRI Kongwa kwa lengo la kuwawezesha vijana na wanawake kujiajiri na kushiriki kikamilifu katika mnyororo wa thamani wa sekta ya mifugo.
Akiwasilisha taarifa ya Mpango na Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2026/2027 leo Mei 14, 2026, katika Kikao cha 29 cha Mkutano wa Tatu wa Bunge la 13 kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema mradi huo utalenga unenepeshaji wa mbuzi kibiashara, uzalishaji wa malisho kwa kutumia teknolojia ya umwagiliaji, pamoja na uchakataji wa vyakula vya mifugo kwa biashara.
Amesema utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuongeza ajira, kuinua kipato na kuongeza tija kwa vijana na wanawake, sambamba na kuchochea maendeleo ya sekta ya mifugo nchini.
