Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI ATEMBELEA TALIRI MPWAPWA
24 Feb, 2025
WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI ATEMBELEA TALIRI MPWAPWA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) leo tarehe 18/02/2025 amefanya ziara ya kutembelea kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Mpwapwa kilichopo Kanda ya Kati mkoani Dodoma kwa lengo la kukagua shughuli zinazofanywa na Taasisi hiyo kituoni hapo ikiwemo malisho na mbegu za malisho kwa ajili ya ustawi wa mifugo nchini.