MKURUGENZI WA TALIRI KANDA YA KATI ATOA ELIMU YA JIWE LISHE
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Kanda ya Kati Dkt. Mwemezi Kabululu akimfungia jiwe lishe la kulamba wanyama mfugaji aliyetembelea banda la taasisi hiyo mara baada ya kumpatia elimu ya jiwe hilo.
Tukio hilo lilifanyika leo tarehe 04/08/2024 viwanja vya Nzuguni Dodoma katika Maonesho ya 31 ya Kilimo ya Kimataifa ambayo kitaifa yanafanyika Kanda ya Kati jijini Dodoma ndani ya viwanja hivyo yakienda sambamba na kauli mbiu isemayo ‘Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi’
TALIRI ni moja kati ya taasisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zinazoshiriki maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu ya teknolojia bora za mifugo zilizoibuliwa na taasisi hiyo ikiwemo elimu ya mbari bora za mifugo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa maziwa, nyama na mazao mengine ya mifugo pamoja na elimu ya mbegu bora za malisho na vyakula vya mifugo kwa wafugaji na wadau wengine wa mifugo.