Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
ELIMU YA UFUGAJI YATOLEWA KWA WAFUGAJI TANGA
16 Oct, 2025
ELIMU YA UFUGAJI YATOLEWA KWA WAFUGAJI TANGA

Bw. Harryson Ihugura Mtafiti Msaidizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) akitoa elimu ya ufugaji bora kwa wafugaji na wadau mbalimbali wa mifugo wanaotembelea banda la taasisi hiyo lililopo katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara jijini Tanga yanapoendelea Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani.

Elimu hiyo ameitoa kupitia teknolojia bora za mifugo zilizozalishwa na taasisi hiyo ikiwemo teknolojia ya malisho na mbegu za malisho, mbari za mifugo na vyakula vya mifugo.