Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
WATAFITI TALIRI TANGA WATOA ELIMU KWA WAFUGAJI
19 Jul, 2024
WATAFITI TALIRI TANGA WATOA ELIMU KWA WAFUGAJI

Katika kuhakikisha changamoto mbalimbali za wafugaji zinaendelea kutatuliwa watafiti kutoka kituo cha TALIRI Tanga kilichopo Kanda ya Mashariki kinachohudumia wafugaji wa mkoa wa Tanga, Dar es salaam, Morogoro na Pwani kimeendelea kutembelea wafugaji mbalimbali kwa lengo la kutoa elimu juu ya ufugaji wenye tija.

Kuanzia tarehe 26/6/2024 hadi 10/07/2024 watafiti hao wamefanikiwa kutembelea wafugaji 200 kutoka Kata 8 za Wilaya ya Muheza na kuwapatia elimu juu ya teknolojia za mifugo zilizoibuliwa na taasisi hiyo pamoja na utunzaji bora wa ndama.

Aidha, jumla ya sampuli 40 za malisho zimechukuliwa kutoka kwa wafugaji hao kwa ajili ya kuzichakata na kubaini ubora wake kabla ya kuwapatia wafugaji hao elimu ya lishe na ulishaji hapo baadae.

Kituo cha TALIRI Tanga kimekuwa na utaratibu wa kutembelea wafugaji ‘out reach program’ kila mwezi kwa lengo la kuwapa elimu ya ufugaji bora, na pia kubaini changamoto za wafugaji na kuzipatia ufumbuzi kwa njia ya tafiti mbalimbali.