Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
TALIRI YANG'ARA KATIKA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA NA KIMATAIFA
10 Aug, 2026
TALIRI YANG'ARA KATIKA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA NA KIMATAIFA

Picha ni tukio linaloonyesha nyuso za furaha na bashasha kwa Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), mara baada ya kupokea tuzo za ushindi katika makundi mbalimbali wakati wa Maonesho ya Kitaifa na Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja mbalimbali vya maonesho vya kikanda nchini.

TALIRI ilishiriki kikamilifu katika maonesho hayo katika kanda mbalimbali nchini, ikionesha teknolojia, ubunifu na matokeo ya tafiti zinazolenga kuendeleza sekta ya mifugo na kuwafikia wafugaji pamoja na wadau mbalimbali.

Katika maonesho hayo, TALIRI ilifanikiwa kupata tuzo mbalimbali, ikiwemo ushindi wa pili katika kundi la Taasisi za Umma zinazotoa Mafunzo na Utafiti, pamoja na ushindi wa tatu katika kundi la Washindi wa Jumla wa Maonesho Ndani ya Uwanja wa Kundi la Mifugo.

Mafanikio haya ni kielelezo cha juhudi, ubunifu, ushirikiano na kujituma kwa Watumishi wa TALIRI katika kuhakikisha utafiti na teknolojia za mifugo zinatumika kuchochea maendeleo ya wafugaji na sekta ya mifugo nchini.

TALIRI — Utafiti kwa Maendeleo ya Sekta ya Mifugo.