Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
TALIRI YAJIPANGA KUTOA ELIMU NA TEKNOLOJIA ZA KISASA ZA MIFUGO KATIKA MAONESHO YA MBOGO RANCHI.
20 Jun, 2026
TALIRI YAJIPANGA KUTOA ELIMU NA TEKNOLOJIA ZA KISASA ZA MIFUGO KATIKA MAONESHO YA MBOGO RANCHI.

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (DGLF), Dkt. Asimwe Rwiguza, akimuelezea Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu namna taasisi zilizo chini ya sekta ya mifugo, ikiwemo Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), zilivyojipanga kutoa elimu na huduma mbalimbali kwa wananchi wanaotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Mifugo na Mnada wa Kimataifa yanayoendelea Mbogo Ranchi, Ubena Zomozi, Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani. Dkt. Rwiguza amesema kuwa TALIRI imejipanga kutoa elimu kuhusu upimaji wa ubora wa maziwa kwa kutumia kifaa cha “Lactoscan”, upimaji wa mabaki ya dawa kwenye maziwa kwa kutumia kifaa cha “Milk Safe Mini Incubator” pamoja na teknolojia za uzalishaji na uhifadhi wa malisho bora kwa ajili ya kuongeza tija katika ufugaji. Maonesho hayo yameandaliwa na Kampuni ya Mbogo Ranchi na yanashirikisha washiriki kutoka Tanzania, Kenya, Namibia na Brazil, huku mgeni rasmi wa uzinduzi akiwa Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba. Juni 19, 2026