TALIRI YAJIPANGA KUTOA ELIMU YA UFUGAJI BORA SABASABA
21 Jul, 2025

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) imejipanga kutoa elimu ya ufugaji bora wa mifugo kwa wadau mbalimbali wa mifugo wanaotembelea banda la taasisi hiyo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwl. J. K. Nyerere jijini Dar es salaam.
Elimu ya teknolojia bora za mifugo zilizozalishwa na taasisi hiyo inaendelea kutolewa kwa wafugaji hao ili kuwezesha ufugaji wenye tija.