TALIRI YASHIRIKI MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) inashiriki Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Usagara Jijini Tanga yakiwa na kaulimbiu isemayo “Tuungane Pamoja Kupata Chakula Bora kwa Maisha Bora ya Baadae”
Pichani ni Bw. Said Abdallah Mbelwa Mtafiti kutoka TALIRI Kanda ya Mashariki akielezea umuhimu wa malisho bora ya mifugo kwa wafugaji na wadau mbalimbali wanaotembelea banda la TALIRI kwa ajili ya kujifunza teknolojia bora za mifugo zinazozalishwa na taasisi hiyo ikiwemo teknolojia bora za malisho, vyakula vya mifugo na mbari bora za mifugo.
Mazao ya mifugo yakiwemo maziwa, nyama na mayai ni moja kati vyakula bora kwa binadamu hivyo, katika maonesho haya TALIRI imejipanga kuelimisha wafugaji kutumia malisho bora ya mifugo na kuzingatia ufugaji wenye tija ili kupata mifugo yenye afya bora na hivyo kuwezesha kupata mazao yenye ubora kwa afya za walaji.