Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
TALIRI YASHIRIKI MAADHIMISHO YA KITAIFA YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, 2026
18 Jun, 2026
TALIRI YASHIRIKI MAADHIMISHO YA KITAIFA YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, 2026


Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) inashiriki Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2026 katika Viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma, yenye kaulimbiu: “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu.”
Katika maonesho hayo, TALIRI inatoa huduma za ushauri wa kitaalamu na majibu ya papo kwa papo kuhusu masuala mbalimbali ya ufugaji na utumishi wa Umma. 
Wageni watapata fursa ya kujifunza kuhusu matokeo ya utafiti, ubunifu na teknolojia za kisasa zinazolenga kuongeza tija katika sekta ya mifugo.
Miongoni mwa teknolojia na elimu zitakazotolewa ni matumizi ya malisho bora, mbegu bora za malisho, mbari bora za mifugo, mbinu za kisasa za ufugaji wenye tija, pamoja na kilimo cha malisho kwa biashara.
Aidha, TALIRI itatoa elimu kuhusu uhifadhi wa malisho, afya ya mifugo, lishe bora kwa mifugo na fursa mbalimbali za uwekezaji na maendeleo katika mnyororo wa thamani wa sekta ya mifugo.
Ewe mfugaji, mdau wa sekta ya mifugo na mwananchi usikose kutembelea banda la TALIRI upate elimu, ushauri wa kitaalamu na teknolojia zitakazokusaidia kuongeza uzalishaji, kuboresha mifugo yako na kuongeza kipato.
TALIRI – Utafiti na Ubunifu kwa Maendeleo ya Mifugo!