Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
GHALA LA KUHIFADHIA MALISHO TALIRI MPWAPWA
01 Apr, 2025
GHALA LA KUHIFADHIA MALISHO TALIRI MPWAPWA

Mradi wa ujenzi wa ghala la kuhifadhia malisho unaotekelezwa kituo cha TALIRI Mpwapwa wenye thamani ya shilingi Milioni 219, ghala hilo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi marobota 30,000 kwa wakati mmoja tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo maghala yaliyopo yalikuwa na uwezo wa kuhifadhi marobota 14,000 pekee.

Ujenzi wa ghala hili utawezesha kuongeza uwezo wa kuhifadhi malisho, kuwezesha upatikanaji wa malisho kwa mwaka mzima, kulinda ubora wa malisho pamoja na kupunguza upotevu wa malisho kutokana na kukosekana kwa mahali pa kuhifadhia malisho hasa kipindi cha masika.