Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
TALIRI YAPATIWA MAFUNZ0 YA MFUMO WA PSSSF MEMBER PORTAL
24 Feb, 2025
TALIRI YAPATIWA MAFUNZ0 YA MFUMO WA PSSSF MEMBER PORTAL

Wataalamu kutoka Mfuko wa Jamii (PSSSF) wametoa mafunzo ya mfumo wa PSSSF Member Portal kwa watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) ikiwa ni wanachama wa mfuko huo lengo likiwa ni kuwawezesha wanachama hao kupata taarifa za mfuko kwa urahisi.

Akitoa mafunzo hayo Majira Werema Afisa kutoka PSSSF ameeleza kuwa mfuko unatoa mafao mbalimbali ikiwemo pensheni za uzee, pensheni ya ulemavu, pensheni ya warithi, mafao ya ugonjwa, mafao ya kukosa ajira na mafao ya uzazi.

Werema ameendelea kueleza kuwa mfuko huo unawajibu wa kulipa mafao kwa usahihi kwa wanachama wake, kuandikisha wanachama, kuwajulisha wadau juu ya mabadiliko ya kimfumo au kisera na kutoa elimu kwa wanachama kuhusu mafao

Sambamba na hayo Werema amewasisitiza wanachama hao kujiandaa kabla ya kustaafu kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kuwekeza kwenye vitega uchumi, kuwa na familia inayoendana na uwezo lakini pia kuzingatia matumizi sahihi ya fedha kulingana na mishahara na kuwekeza kwenye hatifungani za Serikali na mifuko ya umoja UTT.

Akishukuru baada ya mafunzo hayo Hassan Shine amesema mafunzo hayo yataongeza chachu ya kuchukua hatua ya kujiandaa mapema kabla ya kustaafu.