Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
KIKAO CHA UCHAGUZI WA WAJUMBE WA BARAZA DOGO TALIRI MAKAO MAKUU
20 Feb, 2026
KIKAO CHA UCHAGUZI WA WAJUMBE WA BARAZA DOGO TALIRI MAKAO MAKUU

Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Prof. Erick Komba tarehe 17/02/2026 wamefanya kikao cha kuchagua wawakilishi wa wafanyakazi watakaokuwa wajumbe wa baraza dogo la TALIRI Makao Makuu.

Miongoni mwa wajumbe wa baraza hilo ni pamoja na Menejimenti ya TALIRI Makao Makuu, wajumbe kutoka uongozi wa Halmashauri ya Tawi Chama cha wafanyakazi RAAWU na Katibu wa RAAWU Kanda ya Kati.

Akiongea mara baada ya uchaguzi huo Bi. Staile Kiko Katibu wa RAAWU Kanda ya Kati amesema majukumu ya baraza hilo ni kuishauri Menejimenti ya TALIRI Makao Makuu kuhusu masuala mbalimbali ya Taasisi yakiwemo bajeti ya Kituo cha TALIRI Makao Makuu, maslahi ya Wafanyakazi, Mpango wa mafunzo wa Taasisi.

Kwa upande wake Bw. Sabas Mhina Afisa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano amesema uwepo wa mabaraza hayo ni kuhakikisha ushirikishwaji mahala pa kazi unakuwepo ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji kwa watumishi

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Prof. Erick Komba amewataka watumishi hao waliochaguliwa kushirikiana na wajumbe wengine wa baraza hilo kuhakikisha utekelezaji wa shughuli za Taasisi unaimarika na hivyo kufikia malengo ya wafugaji na wadau wengine wa mifugo.

Watumishi waliochaguliwa katika kikao hicho ni pamoja na Mohamed Nayana, Hadija Swalehe, Neema Mkama na Janeth Vedastus ambapo kati yao Neema Mkama amechaguliwa kuwa mwakilishi wa Wafanyakazi katika Baraza kuu la Wafanyakazi wa TALIRI.

Ifahamike kuwa msimamizi Mkuu wa mabaraza ya Wafanyakazi nchini ni Kamishna wa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano.