Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
WATUMISHI TALIRI WAKUTANA KUJADILI MASUALA YA TAASISI
24 Feb, 2025
WATUMISHI TALIRI WAKUTANA KUJADILI MASUALA YA TAASISI

Leo tarehe 29/01/2024 wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Makao Makuu wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Prof. Erick Komba wamekutana kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji kwa lengo kuimarisha utendaji kazi wa watumishi hao.

Katika kikao hicho Prof. Komba amewataka watumishi hao kuendelea kuwa waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuwezesha utoaji wa huduma bora za taasisi kwa wananchi wanaojishughulisha na ufugaji.

Sambamba na hayo Prof. Komba amewasisitiza watumishi hao kuendelea kusimamia misingi bora ya uwajibikaji kwa Umma kwa kuzingatia kanuni za maadili ya utumishi wa Umma na kuwataka kufanya kazi kwa bidii ili kutoa matokeo yanayotarajiwa kwa maslahi ya wafugaji na Taifa kwa ujumla.

Akifafanua kanuni hizo Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi TALIRI Bi. Joyce Sakaya ameeleza kuwa kila mtumishi anapaswa kuwa na malengo mahususi ya utendaji kazi, utii wa sheria, bidii ya kazi, kutoa huduma bila upendeleo, kufanya kazi kwa uadilifu, kuwajibika kwa Umma, kuheshimu sheria na kuwa na matumizi sahihi ya taarifa.

Kikao hicho kililenga kuongeza uwajibikaji kwa watumishi na kuwapa fursa ya kutoa maoni yenye kujenga kwa lengo la kuboresha ufanisi wa Taasisi.