Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
WATUMISHI TALIRI WASHAURIWA KUPIMA AFYA ZAO
01 Dec, 2025
WATUMISHI TALIRI WASHAURIWA KUPIMA AFYA ZAO

Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) wameshauriwa kuwa na desturi za kupima afya zao mara kwa mara ili kutambua hali zao na hivyo kujilinda dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Hayo yameelezwa na Dkt. Masoud Ntiga Mratibu wa UKIMWI na magonjwa ya ngono na homa ya ini kutoka ofisi ya mganga mkuu halmashauri ya jiji la Tanga wakati akitoa elimu juu ya UKIMWI, ambapo amesema kuwa zipo njia nyingi za kupata ugonjwa huo kama vile kushiriki ngono zembe, maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua au kunyonyesha, maambukizi wakati wa kuongezewa damu na kuchangia vitu vyenye ncha kali kama vile sindano (hususani kwa waraibu wa madawa ya kulevya).

Dkt. Ntiga ameendelea kueleza kuwa makundi hatarishi ambayo yapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi ni waraibu wa madawa, wanawake au wanaume wenye tabia hatarishi hasa wanaofanya biashara ya ngono.

“Ni muhimu sana kila mara tupime afya zetu ili kujua hali zetu na kuendelea kuchukua tahadhari kubwa kwa kuepuka vishawishi na njia zote zinazopelekea kupata maambukizi.” Amesema Dkt. Ntiga.

Mwisho Dkt. Ntiga ameeleza katika jitihada za kufikia malengo ya kutokomeza ugonjwa wa UKIMWI kila mwaka tarehe 1 Desemba hufanyika maadhimisho ya siku ya UKIMWI na kwa kauli mbiu ya mwaka huu ni “SHIND