MKURUGENZI TALIRI ATOA ELIMU YA MIFUGO, SABASABA
19 Jul, 2024

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Prof. Erick Komba (kushoto), akitoa elimu ya teknolojia za mifugo zilizoibuliwa na taasisi hiyo ikiwemo ya malisho bora, mbari bora na jiwe lishe kwa mdau aliyetembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. Julius Nyerere, Dar es salaam.