Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
TALIRI YAENDELEA KUTOA ELIMU YA UFUGAJI BORA KWA WANANCHI SABASABA
02 Jul, 2026
TALIRI YAENDELEA KUTOA ELIMU YA UFUGAJI BORA KWA WANANCHI SABASABA

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) imeendelea kutoa elimu ya ufugaji bora kwa wananchi wanaotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Wananchi hao wamepata elimu juu ya lishe bora ya mifugo, uboreshaji wa vinasaba, udhibiti wa magonjwa, matumizi ya teknolojia mbalimbali za ufugaji zilizozalishwa na Taasisi hiyo kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya sekta ya mifugo nchini.

Elimu hiyo inalenga kuwawezesha wafugaji na wadau wa sekta ya mifugo kutumia teknolojia na mbinu za kisasa ili kuongeza uzalishaji na tija.

Aidha, wananchi wanapata fursa ya kuuliza maswali na kupata ushauri wa kitaalamu unaozingatia mahitaji yao.

TALIRI inaendelea kuwakaribisha wananchi wote kutembelea banda hilo ili kujifunza, kupata ushauri wa kitaalamu na kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo.