Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
VITUO TALIRI VYATAKIWA KUJIENDESHA KIBIASHARA.
27 Nov, 2025
VITUO TALIRI VYATAKIWA KUJIENDESHA KIBIASHARA.

VITUO TALIRI VYATAKIWA KUJIENDESHA KIBIASHARA.

Vituo vya Kanda vya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) vimetakiwa kuwa na mtazamo wa kibiashara ili kuweza kutimiza malengo ya utafiti na kukuza uchumi wa Taasisi na Taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Andrew Chota wakati wa kikao kazi cha kusikiliza changamoto, kupokea maoni na kueleza musuala ya kiutumishi na kitafiti kwa watumishi wa TALIRI Kanda ya Kati kituo cha Mpwapwa.

“Taasisi inazalisha teknolojia bora za mifugo hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunazitumia kuboresha uzalishaji wa ndani ya Taasisi na kuzipeleka sokoni kwa wananchi ili Taasisi ipate mapato na kukuza uchumi na wanachi wapate mifugo na malisho yanayoongeza tija ya ufugaji na hivyo kuongeza kipato cha familia” amesema Dkt. Chota.

Ameendelea kueleza “Haina haja ya kuwa na mifugo mingi ambayo hatuifanyii tena utafiti wakati wananchi wanahitaji bidhaa hizo. Tukiwa na mtazamo wa kibiashara tutaongeza uzalishaji na kupata fedha ambazo zitasaidia katika shughuli za uendeshaji wa kila siku hivyo hili ni jukumu letu sote kuhakikisha hilo Jambo linatimia Taasisi yetu ina watumishi wenye uwezo tena vijana ambao tunategemea watakuwa chachu ya utendaji kazi ili kutimiza dira na malengo ya taasisi”

Pamoja na hayo Dkt Chota amewahimiza watafiti kuongeza kasi ya kuandika miradi ya kitafiti ili kupata fedha kwa ajili ya utafiti wa teknolojia mbalimbali za mifugo zitakazoboresha sekta ya mifugo nchini na hivyo kukuza uwezo wa kiuchumi wa Taasisi na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Afisa rasilimali watu kutoka TALIRI Bi. Odilia Malenga akielezea masuala ya kiutumishi amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi na bidii ili kuiwezesha Taasisi kutimiza malengo yake.

“Wote tupo hapa kuwahudumia wananchi, hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunatimiza wajibu huo ikiwa ni pamoja na kutunza mali na mapato ya taasisi na kuepuka ubadhilifu na matumizi mabaya ya rasilimali zetu kwani kufanya hivyo ni kosa kimaadili na kisheria.” Ameeleza Odilia