Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
MAABARA YA LISHE YA MIFUGO TALIRI KUHAKIKISHA UBORA WA CHAKULA
16 Oct, 2025
MAABARA YA LISHE YA MIFUGO  TALIRI KUHAKIKISHA UBORA WA CHAKULA

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) imeendelea kutoa elimu ya ufugaji bora kwa wafugaji wanaotembelea banda la TALIRI lililopo ndani ya viwanja vya Shule ya Sekondari ya Usagara jijini Tanga yanapoendelea Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani.

Maonesho hayo yanaenda sambamba na kaulimbiu isemayo “Tuungane Pamoja Kupata Chakula Bora kwa Maisha Bora”

Katika kuhakikisha ubora wa chakula unaimarika kwa ajili ya maisha bora ya wananchi (walaji wa mazao ya mifugo hususani maziwa na nyama) TALIRI kupitia Maabara yake ya Lishe ya Wanyama imeendelea kuhakikisha mazao hayo yanakuwa salama kwa kuchunguza ubora wa malisho anayopewa mnyama pamoja na kupima maziwa ili kuangalia mabaki ya madawa aliyopewa mnyama kama yapo kwenye maziwa.

Tembelea banda la TALIRI ujinze mambo mengi mazuri juu ya ufugaji wenye tija unaozingatia afya ya watumiaji wa mazao ya mifugo na kuzifahamu teknolojia bora za mifugo zilizozalishwa na Taasisi hiyo.