Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
TALIRI NA TAFITI ZA MNYAMA KAZI PUNDA
16 Dec, 2024
TALIRI NA TAFITI ZA MNYAMA KAZI PUNDA

Mbali na tafiti kwa wanyama wengine wafugwao ambazo Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) imekuwa ikifanya, taasisi hiyo pia inafanya tafiti juu ya mnyama punda.

Utafiti umebaini kuwa punda ni moja ya wanyama wenye mzunguko mrefu wa uzazi kutokana na kuwa na kipindi kirefu cha kubeba mimba takribani miezi 10 - 12 na kulea mtoto kwa muda mrefu takribani miezi 7 hii inapelekea kuwepo na idadi ndogo ya punda nchini hivyo tafiti zaidi zinaendelea za kuona namna ya kukabiliana na hili.

Lakini pia miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya nyama na ngozi ya punda kitendo ambacho kinapelekea punda kuzidi kupungua na kusababisha wasiwasi kwa ustawi wa punda na maisha ya jamii za vijijini ambazo zinategemea punda kwa maendeleo ya uchumi.

Msimamo wa Serikali ni kuwa punda si mnyama wa kuliwa bali atumike kama mnyama kazi na kwa kuzingatia ustawi wake na kumhudumia kama ilivyo kwa mifugo mingine.

Kihistoria matumizi makubwa ya punda yamekuwa ni kwa ajili ya usafiri wa kuaminika zaidi ambapo wanaweza kufika hata kwenye ardhi yenye miinuko mikali ambayo ni vigumu kwa gari au trekta kufika, lakini pia tafiti zinaonesha kuwa punda anauwezo wa kulima takribani ekari moja kwa siku kwenye ardhi tambarare.

#PundaWanguMaishaYangu.
#MuuwePundaUwePundaWewe.
#tariliutafitikwamaendeleo