TALIRI yaona mwanga wa mafanikio kupitia ushirikiano na Teagasc ya Ireland

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) inajivunia ushirikiano na msaada madhubuti kutoka kwa Taasisi ya Kilimo na Maendeleo ya Chakula ya Ireland (Teagasc). Ushirikiano huu umeleta matumaini mapya ya mafanikio katika kuboresha vinasaba vya ng’ombe wa maziwa nchini, hasa kupitia upatikanaji wa malisho bora yaliyostawi vizuri mashambani.Pichani ni ndama waliopo kwenye padoki zilizozungushiwa uzio, katika shamba la malisho aina ya Cenchrus ciliaris, ikiwa ni sehemu ya uwekezaji wa Mradi wa Maziwa Faida. Mradi huu unalenga kuongeza mnyororo wa thamani wa ng’ombe wa maziwa nchini, na unatekelezwa na Kituo cha Utafiti cha TALIRI Tanga kwa ufadhili wa Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania.Ndama wanaozaliwa kituoni hapo hutunzwa kwa umakini mkubwa na hufuatiliwa kwa ukaribu katika kila hatua ya malezi yao, ili kuhakikisha wanakua kuwa ng’ombe bora wa maziwa kwa manufaa ya wafugaji wa Kitanzania.
Maziwa Faida ni tumaini jipya kwa ufugaji endelevu wa ng’ombe wa maziwa nchini Tanzania.