Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
WADAU WAENDELEA KUPATA ELIMU YA MIFUGO, TALIRI
19 Jul, 2024
WADAU WAENDELEA KUPATA ELIMU YA MIFUGO, TALIRI

Wadau wa Sekta ya Mifugo wameendelea kupatiwa elimu ya teknolojia za mifugo zilizoibuliwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kutoka kwa watafiti wa taasisi hiyo katıka Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es salaam ndani ya banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi yakiwa sambamba na kauli mbiu isemayo “Tanzania: Mahali Sahihi pa Biashara na Uwekezaji”