MDAU APATIWA ELIMU YA NYASI AINA YA MAJANI YA TEMBO

Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Walter Mangesho akitoa maelezo ya upandaji wa nyasi aina ya majani ya tembo ‘Napier’ kwa mdau wa Sekta ya Mifugo alipotembelea banda la TALIRI katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam.
Mangesho ameeleza kuwa nyasi hizo zina kiwango cha protini cha asilimia 12 na hivyo kuwezesha mifugo hususani mifugo ya wanyama wanaocheu akiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo kuongeza virutubisho.
Sambamba na hayo Mangesho ameeleza kuwa nyasi hizo zinaweza kupandwa kwa kukata pingili ambapo pingili 4000 zinaweza kuoteshwa kwenye shamba la ekari moja na kumuwezesha mfugaji kupata mavuno ya tani 8 - 16 ya majani mabichi kwa ekari kwa mwaka ambayo itatosha kulisha ng’ombe 1 - 2 kwa mwaka.
Tembelea banda la TALIRI kujifunza ufugaji wenye tija.