Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
KUTOKA LITA 7 HADI 15 KWA SIKU, MRADI WA MAZIWA FAIDA WABADILISHA MAISHA YA WAFUGAJI MUHEZA
18 May, 2026
KUTOKA LITA 7 HADI 15 KWA SIKU, MRADI WA MAZIWA FAIDA WABADILISHA MAISHA YA WAFUGAJI MUHEZA

“Mradi wa Maziwa Faida umeleta mapinduzi makubwa kwa ufugaji wetu. Kabla ya kupata mafunzo nilikuwa nafuga kimazoea na nilidhani ng’ombe wangu hawana tija. Kupitia elimu ya ufugaji bora nimegundua kuwa tatizo halikuwa ng’ombe, bali namna ya utunzaji. Leo hii ng’ombe aliyekuwa akinipa lita 6 hadi 7 za maziwa kwa siku, sasa anatoa hadi lita 15 kwa siku kutoka kwa ng’ombe huyo huyo.

Kwetu sisi wafugaji, Mradi wa Maziwa Faida ni mkombozi wa kweli.” Siwema Kihenya, mfugaji kutoka Muheza, Tanga.

Nawe ni mfugaji unatamani kufanikiwa kama Siwema?

Usikose kushiriki Siku ya Maonesho ya Ubunifu na Teknolojia katika Sekta ya Maziwa - TALIRI Open Day 2026 itakayofanyika tarehe 11/06/2026 katika viwanja vya TALIRI Tanga.

Utajifunza mbinu za kisasa za ufugaji wa ng’ombe wa maziwa, utakutana ana kwa ana na wataalamu wa mifugo na utapata suluhisho halisi kwa changamoto zako za ufugaji.

Karibu sana!

“TALIRI - Utafiti kwa Maziwa Zaidi”

Maziwa Faida ni Mradi unaolenga kuboresha mnyororo wa thamani kwa ng’ombe wa maziwa unaotekelezwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Kanda ya Mashariki kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti, Ushauri na Mafunzo ya Kilimo na Chakula nchini Ireland kupitia ufadhili wa Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania.