Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
MKUU WA MKOA WA KIGOMA ATEMBELEA TALIRI NSIMBO, NANENANE
06 Aug, 2024
MKUU WA MKOA WA KIGOMA ATEMBELEA TALIRI NSIMBO, NANENANE

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amefurahishwa kwa namna Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) ilivyojipanga katika utoaji wa elimu ya ufugaji bora kwa wadau mbalimbali wa mifugo.

Mhe. Andengenye ameeleza kufurahishwa huko alipotembelea banda la TALIRI Kanda ya Magharibi katika Maonesho ya 31 ya Kilimo ya Kimataifa (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Ipuli mkoa wa Tabora kwa lengo la kujionea teknolojia mbalimbali za mifugo zilizoibuliwa na taasisi hiyo.

Vilevile Mhe. Andengenye ameeleza kuwa TALIRI ni taasisi muhimu kwa wafugaji na wadau wa mifugo kwani inatoa fursa kwa wafugaji kufanya ufugaji wenye tija kwa kuzingatia elimu ya ufugaji bora na matumizi ya teknolojia bora za mifugo zilizoibuliwa na taasisi hiyo.

Sambamba na hayo Mhe. Andengenye ameitaka taasisi hiyo kuendelea kusambaza elimu ya upandaji wa malisho bora kwa wafugaji ili kupunguza migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.