Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
TAKUKURU WATEMBELEA TALIRI
26 Nov, 2024
TAKUKURU WATEMBELEA TALIRI

Leo tarehe 19/11/2014 Wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) wamepatiwa elimu juu ya masuala ya rushwa mahali pa kazi na Maafisa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) lengo ikiwa ni kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu.

Akiongea Lilian Lyimo Afisa kutoka TAKUKURU amesema rushwa mahali pa kazi ni matumizi mabaya ya ofisi ya Umma kwa manufaa binafsi ambayo hupelekea kukosekana kwa haki kwa anaestahili, kuisababishia Serikali hasara na jamii kwa ujumla, miradi isiyokuwa na ubora unaotakiwa, ununuzi wa vifaa hewa au visivyo na viwango na kuwepo kwa matabaka na chuki miongoni mwa watumishi.

Liliani ameendelea kueleza kuwa kila mtumishi anapaswa kuzingatia kanuni za maadili ya utumishi ikiwemo kutoa huduma bora, utii wa Serikali, bidii ya kazi, kutoa huduma bila upendeleo, kufanya kazi kwa uadilifu, kuwajibika kwa Umma, kuheshimu sheria na matumizi sahihi ya taarifa ili kuepukana na rushwa.

“Rushwa ni adui wa haki tushirikiane kuitokomeza” aliongeza Liliani.

Aidha, Lilian ameeleza kuwa TAKUKURU inajukumu la kuzuia na kupambana na rushwa na inafanya hivyo kwa kuelimisha Umma juu ya masuala ya rushwa, kufanya utafiti na kubaini mianya ya rushwa, kufuatilia fedha za miradi ya maendeleo, kufanya uchunguzi na kufikisha watuhumiwa mahakamani.

Kwa upande wake Gilbert Msuta Kaimu Mkurugenzi wa TALIRI amesema anashukuru kwa elimu hiyo muhimu yenye lengo la kuongeza uwajibikaji unaotakiwa katika utekelezaji wa majukumu na kwamba TALIRI itaendelea kutoa huduma bora kwa jamii bila kuruhusu mianya ya rushwa.