UZALISHAJI WA MBEGU ZA MALISHO WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 85.5
Uzalishaji wa mbegu za malisho nchini umeongezeka kwa asilimia 85.5 kutoka tani 222.54 mwaka wa fedha 2024/2025 hadi tani 411.25 mwaka 2025/2026 katika mashamba ya Serikali na binafsi, zenye thamani ya Shilingi bilioni 1.78.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka 2025/2026 ya Wizara hiyo, leo Mei 14, 2026, katika Kikao cha 29 cha Mkutano wa Tatu wa Bunge la 13 kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa, Bungeni jijini Dodoma.
Taarifa hiyo iliwasilishwa ikiwa ni sehemu ya mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ambapo Serikali imeendelea kusisitiza uwekezaji katika uzalishaji wa malisho ili kuongeza tija katika sekta ya mifugo nchini.
