WASHIRIKI WA WARSHA YA TDGG WAJADILI UTAYARI WA UPANUZI WA MFUM
Washiriki wa Warsha ya Mradi wa Kuboresha Vinasaba vya Ng’ombe wa Maziwa katika Ukanda wa Kitropiki (TDGG) inayoendelea katika ukumbi wa Hoteli ya Panama mkoani Kilimanjaro leo Juni 24, 2025 wameendelea na siku ya pili ya warsha hiyo kwa kujadili na kutathmini kiwango cha utayari wa upanuzi wa Mfumo wa TDGG, kwa lengo la kuharakisha matumizi yake kwa kiwango kikubwa.
Katika kikao hicho, washiriki walifanya uchambuzi wa kina wa huduma mbalimbali za mfumo kwa kuzingatia ubunifu unaohitajika, maeneo yenye vikwazo na hatua zilizofikiwa katika utekelezaji.
Aidha, washiriki walibainisha changamoto zinazoweza kuathiri upanuzi wa matumizi ya mfumo na kupendekeza mikakati mbalimbali itakayosaidia kuimarisha utekelezaji na kuongeza tija katika sekta ya maziwa.
Uchambuzi huo unatarajiwa kutoa taarifa muhimu zitakazosaidia kubainisha hatua mahsusi zinazopaswa kuchukuliwa ili kuharakisha maendeleo na kuhakikisha mfumo wa TDGG unatumika kwa ufanisi zaidi katika kuboresha vinasaba vya ng’ombe wa maziwa nchini.
