NIC WATEMBELEA TALIRI
Tarehe 19/11/2024 wataalamu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wametembelea Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa lengo la kuwaelezea watumishi wa taasisi hiyo juu ya huduma za bima zinazotolewa na shirika hilo.
Shirika hilo linatoa huduma mbalimbali za bima ikiwemo bima za mali, ajali, ujenzi, maisha na bima ya kilimo na mifugo.
Wataalamu hao wakiongozwa na Meneja wa Kanda ya Kati wa Shirika hilo Alex Suzuguye wamesema tofauti ya bima zinazotolewa na shirika hilo na bima zingine ni uharaka wa mteja kupata huduma stahiki na kwa wakati pale inapohitajika lakini pia shirika hilo linahuduma zingine za bima ambazo hazipatikani kwenye ofisi zingine za bima ikiwemo bima ya Kilimo na Mifugo.
Aidha, wametoa wito kwa watumishi hao kuwa wazalendo kwa kukata bima za shirika hilo la kiserikali kwa maslahi ya Taifa na usalama wa mali zao na maisha kwa ujumla.