HABARI PICHA :TALIRI WAAHIDI USHIRIKIANO THABITI KATIKA UTEKELEZAJI WA MRADI WA STE & GRL
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Andrew Chota akiwasilisha ujumbe wa TALIRI wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kusaidia Uhifadhi wa Mfumo Ikolojia wa Tanganyika na Urejeshaji wa Malisho (STE & GRL), uliofanyika tarehe 21 Oktoba 2025, Mkoa wa Katavi.
Dkt. Chota amesisitiza kuwa TALIRI imejipanga kushirikiana kwa karibu na wadau wote wa mradi huu, ili kuhakikisha malengo ya mradi yanafikiwa kwa ufanisi.
Ameongeza kuwa taasisi hiyo itatumia uzoefu wake katika tafiti za mifugo, uhifadhi wa mazingira na urejeshaji wa malisho ili kusaidia kutatua changamoto zinazotokana na uhamaji wa wakulima na wafugaji, na hivyo kuboresha uhusiano wa kijamii, kiuchumi na kiikolojia katika Wilaya ya Tanganyika.
