Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
MRATIBU WA MRADI WA STE & SGR PROF. THEOBALD KUTOKA MZUMBE AKIFAFANUA MALENGO YA MRADI
28 Oct, 2025
MRATIBU WA MRADI WA STE & SGR PROF. THEOBALD KUTOKA MZUMBE AKIFAFANUA MALENGO YA MRADI



Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Uhifadhi wa Mfumo Ikolojia wa Tanganyika na Urejeshaji wa Malisho (STE & GRL) kwa upande wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Frank Theobald, akielezea kuhusu asili (genesis), lengo na matarajio ya utekelezaji wa mradi huo wakati wa uzinduzi uliofanyika tarehe 21 Oktoba 2025, Wilayani Tanganyika, Mkoa wa Katavi.

Prof. Theobald amefafanua kuwa mradi huu unalenga kuimarisha ustahimilivu wa jamii za wakulima na wafugaji kupitia uhifadhi endelevu wa mazingira, urejeshaji wa malisho, na matumizi bora ya ardhi, ili kukuza ustawi wa kijamii na kiuchumi wa wananchi wa eneo hilo. Pia, kupitia mradi huu, shamba darasa litaanzishwa ili kutoa elimu ya vitendo kwa wadau kuhusu mbinu bora za kilimo na ufugaji rafiki wa mazingira.

Tukio hilo limehusisha wadau kutoka TALIRI, COSTECH, Chuo Kikuu Mzumbe, Maafisa Ugani, Maafisa Kilimo na Mifugo, pamoja na viongozi wa vijiji na kata wa Wilaya ya Tanganyika.