Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
HABARI PICHA: MZUMBE KUSAIDIA UHIFADHI WA MAZINGIRA KUPITIA MRADI WA STE & GRL
05 Nov, 2025
HABARI PICHA: MZUMBE KUSAIDIA UHIFADHI WA MAZINGIRA KUPITIA MRADI WA STE & GRL

Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Nsubili Isaga, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kusaidia Uhifadhi wa Mfumo Ikolojia wa Tanganyika na Urejeshaji wa Malisho (STE & GRL), uliofanyika tarehe 21 Oktoba 2025, Mkoa wa Katavi. Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa taasisi nne: Chuo Kikuu Mzumbe, TALIRI, COSTECH na NORAD (Norway)

Dkt. Isaga ameeleza kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kinathamini kwa dhati ushiriki wake katika utekelezaji wa mradi huu, ambao unaendana na dhamira ya Chuo katika kuchangia maendeleo endelevu ya jamii kupitia utafiti, ushauri na elimu bunifu. Ameongeza kuwa chuo kimejipanga kushirikiana kwa karibu na wadau wote ili kuhakikisha matokeo ya mradi yanawanufaisha moja kwa moja wananchi wa eneo husika.

Amesisitiza kuwa mradi huu ni mfano halisi wa namna ambavyo taasisi za elimu ya juu zinavyoweza kuchangia katika kulinda mazingira, kukuza uchumi wa kijamii na kuhimiza matumizi endelevu ya rasilimali asilia kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.