HABARI PICHA: UZINDUZI WA MRADI WA STE & GRL – KATAVI
Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kimezindua rasmi Mradi wa Kusaidia Uhifadhi wa Mfumo Ikolojia wa Tanganyika na Urejeshaji wa Malisho (STE & GRL), unaofadhiliwa na Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Norway (Norad) na kuratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Uzinduzi huu umefanyika tarehe 21 Oktoba 2025, Mkoani Katavi, ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Mhe. Onesmo Buswelu, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko.
Mradi huu utakaotekelezwa kwa miaka mitatu unalenga kuboresha ustawi endelevu wa maisha kupitia uhifadhi wa mazingira, usimamizi wa malisho, na kuimarisha ushirikiano wa wadau wa kilimo, mifugo na uhifadhi katika Wilaya ya Tanganyika, Mkoani Katavi.
