HABARI PICHA
01 Nov, 2024

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Kanda ya Mashariki Dkt. Zabron Nziku (aliyesimama) akielezea shughuli zilizofanywa hadi sasa kupitia utekelezaji wa Mradi wa Maziwa Faida kwa Viongozi wa Ubalozi wa Ireland Nchini Tanzania wakiongozwa na Naibu Mkuu wa Ushirikiano Hellen Counihan (hayupo pichani) leo terehe 23/10/2024 walipotembelea Ofisi za kanda hiyo zilizopo Mkoani Tanga kwa lengo la kujionea namna Taasisi hiyo inavyotekeleza Mradi wa Maziwa Faida unaofadhiliwa na Ubalozi huo.