HABARI PICHA
01 Nov, 2024

Mfugaji kutoka Wilaya ya Muheza Edna Nkya (wa pili kushoto) akielezea kwa Viongozi wa Ubalozi wa Ireland Nchini Tanzania walipotembelea Ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kanda ya mashariki, namna mradi wa maziwa faida umemuwezesha kupata elimu ya ufugaji bora kitendo ambacho kimemfanya aweze kumudu gharama za maisha kutokana na ongezeko kubwa la maziwa anayoyapata kutoka kwa ng’ombe wake tofauti na ilivyokuwa hapo awali.