Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
HABARI PICHA
24 Feb, 2025
HABARI PICHA

Picha mbalimbali zikimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Burian (mwenye ushungi mweusi) leo tarehe 29/01/2025 akiongoza zoezi la uvunaji wa mbegu za malisho aina ya _Cenchrus Ciliaris_ kwenye shamba la malisho hayo lililopo Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Kanda ya Mashariki Mkoani Tanga.

Uvunaji huo umejumuisha wataalamu kutoka taasisi hiyo, wafugaji na viongozi wengine alioambatana nao.

Nae Mkurugenzi wa TALIRI Kanda ya Mashariki Dkt. Zabron Nziku ameshiriki zoezi hilo.