Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
HABARI KATIKA PICHA
01 Nov, 2024
HABARI KATIKA PICHA

PICHA NA 1 (YA JUU):
Mratibu wa Mradi wa AADGG Kitaifa Dkt. Eliamoni Titus Lyatuu akielezea shughuli zinazoendelea kutekelezwa kupitia mradi wa ‘African Asia Diary Genetic Gain - AADGG’ wa kuboresha mbari za ng’ombe wa maziwa kwa Maafisa ugani wa Mikoa saba ambayo mradi huo unatekelezwa kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) katika mafunzo ya mfumo wa kidigitali wa kukusanya takwimu za mradi huo yanayotolewa kwa maafisa ugani hao katika ukumbi wa African Dreams Hotel Mkoani Dodoma.

PICHA NA 2 (YA CHINI KUSHOTO):
Neema Kelya Afisa TEHAMA wa Mradi wa Kuboresha Mbari Bora za Ng’ombe wa Maziwa kupitia Mradi wa ‘African Asia Diary Genetic Gain - AADGG’ akitoa mafunzo ya jinsi ya kutumia Mfumo wa Kidijitali wa Kukusanya Takwimu za mradi huo kwa Maafisa Ugani wa Mikoa saba ambayo inatekeleza mradi huo chini ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) na Kituo cha Taifa cha Uhaulishaji (NAIC). Mikoa hiyo ni pamoja na Mkoa wa Mbeya, Njombe, Songwe, Iringa, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

PICHA NA 3 (YA CHINI KULIA):

Maafisa Ugani wakipatiwa mafunzo ya Mfumo mpya wa Kidijitali wa kukusanya takwimu za mradi wa kuboresha mbari bora za ng’ombe wa maziwa kupitia mradi wa ‘African Asia Diary Genetic Gain - ADGG’ unaotekelezwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) na Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC).