BI. NEEMA KYELA AWASILISHA MADA KUHUSU MFUMO WA TDGG
25 Jun, 2026
Afisa TEHAMA wa Mradi wa Kuboresha Vinasaba vya Ng’ombe wa Maziwa katika Ukanda wa Kitropiki (TDGG) kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) Bi. Neema Keyla, akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa TDGG unaowezesha ukusanyaji, uhifadhi, uchambuzi na matumizi ya taarifa za mifugo kwa njia ya kidijitali, wakati wa warsha ya wadau wa sekta ya mifugo iliyofanyika Juni 23, 2026 katika ukumbi wa Panama Hoteli mkoani Kilimanjaro.
