MOLASI KUONGEZA LADHA NA NGUVU KWENYE CHAKULA CHA MIFUGO

Mkurugenzi wa Utafiti wa Mifugo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Dkt. Andrew Chota akiweka Molasi ‘Molasses’ kwenye chakula cha ng’ombe waliopo banda la taasisi hiyo lililopo viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma kwenye maonesho ya Nanenane kwa lengo la kumuongezea ladha na viini lishe muhimu vya kumpatia nguvu.
Molasi ni bidhaa inayopatikana wakati wa uchakataji wa miwa ili kupata sukari.
TALIRI ni moja kati ya taasisi zinazoshiriki Maonesho ya 31 ya Kilimo ya Kimataifa ‘Nanenane’ yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma yakiwa na kauli mbiu isemayo “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”
Tembelea banda la TALIRI ujifunze teknolojia mbalimbali za mifugo zilizozalishwa na taasisi hiyo.