WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUTUMIA SHILINGI BILIONI 433.3 KWA MWAKA 2026/2027
WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUTUMIA SHILINGI BILIONI 433.3 KWA MWAKA 2026/2027
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imepanga kutumia shilingi bilioni 433.3 katika mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya kuimarisha sekta za mifugo na uvuvi nchini.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Wizara hiyo, Mheshimiwa Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (Mb) wakati akiwasilisha taarifa ya mpango na bajeti ya wizara hiyo leo Mei 14, 2026 katika Kikao cha 29 cha Mkutano wa 3 wa Bunge la 13 uliofanyika Ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma.
Amesema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 98.2 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, huku shilingi bilioni 335 zikielekezwa kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Aidha, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amefafanua kuwa kati ya fedha za matumizi ya kawaida, shilingi bilioni 49.4 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi na shilingi bilioni 48.8 zitatumika kugharamia matumizi mengineyo ya uendeshaji wa shughuli za wizara.
Kwa upande wa bajeti ya maendeleo, amesema shilingi bilioni 193.7 zinatarajiwa kutoka katika vyanzo vya ndani, huku shilingi bilioni 141.3 zikitarajiwa kutoka kwa wadau wa maendeleo.
Ameongeza kuwa bajeti hiyo itatekelezwa kwa kuzingatia vipaumbele mbalimbali ikiwemo kuongeza uzalishaji, kuimarisha masoko na kuongeza thamani ya mazao ya mifugo na uvuvi, pamoja na kuimarisha ulinzi na usimamizi wa rasilimali za sekta hizo.
Vipaumbele vingine ni kuhamasisha uwekezaji katika sekta za mifugo na uvuvi, pamoja na kuimarisha utafiti, mafunzo na huduma za ugani ili kuongeza tija kwa wafugaji na wavuvi nchin
