Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA, KILIMO NA MIFUGO WAPATIWA MBUZI.
24 Feb, 2025
WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA, KILIMO NA MIFUGO WAPATIWA MBUZI.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Prof. Erick Komba akiongoza zoezi la ugawaji wa madume ya mbuzi walioboreshwa aina ya Malya kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo lengo ikiwa ni kuendelea kusambaza teknolojia bora za mifugo kwa wafugaji na wadau mbalimbali wa mifugo.

Madume hayo ya mbuzi yatatumika kuwapanda mbuzi wa asili wa wajumbe hao ili kuboresha uzao kwani vitoto vitakavyozaliwa vitakuwa ni bora.