Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO ATEMBELEA BANDA LA TALIRI
06 Aug, 2024
MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO ATEMBELEA BANDA LA TALIRI

Katika Maonesho ya 31 ya Kilimo ya Kimataifa Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma yakiwa na kauli mbiu isemayo ‘Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi’ leo tarehe 03/08/2024 Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamo - Hanga (kulia) ametembelea banda la Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kupata elimu juu ya ufugaji bora.

Akiwa ndani ya banda hilo Nyamo - Hanga amepata elimu ya mbari bora za mifugo kwa lengo kuongeza uzalishaji wa maziwa, nyama na mazao mengine ya mifugo pamoja na elimu ya mbegu bora za malisho na vyakula vya mifugo ikiwa ni teknolojia za mifugo zilizoibuliwa na taasisi hiyo kutoka kwa Afisa Mifugo wa taasisi hiyo Ndg. Salome Nyabusani (kushoto)

Aidha, Salome ameeleza namna ng’ombe aina ya Mpwapwa anavyoweza kuhimili mazingira yenye ukame.