Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
WADAU WA MIFUGO WATEMBELEA BANDA LA TALIRI KANDA YA ZIWA
05 Aug, 2024
WADAU WA MIFUGO WATEMBELEA BANDA LA TALIRI KANDA YA ZIWA

Katika Maonesho ya 31 ya Kilimo ya Kimataifa (Nanenane) yanayoendelea Kanda ya Ziwa katika viwanja vya Nyamhongolo mkoa wa Mwanza ambayo kitaifa yanafanyika Dodoma viwanja vya Nzuguni yakiwa na kauli mbiu isemayo ‘ Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi’

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Kanda ya Ziwa kituo cha Mabuki imefanikiwa kushiriki maonesho hayo ambapo elimu ya teknolijia bora za mifugo zilizoibuliwa na taasisi hiyo zimeendelea kutolewa kwa wadau mbalimbali wa mifugo wanaotembelea banda la TALIRI ndani ya viwanja vya Nyamhongolo, Mwanza