WADAU WA MIFUGO WAPATIWA ELIMU YA MALISHO BORA
19 Jul, 2024

. Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Ezekiel Maro (kulia) akielezea masuala ya malisho bora ya mifugo ikiwa ni moja kati ya teknolojia zilizoibuliwa na taasisi hiyo kwa mdau wa sekta ya mifugo alipotembelea banda la TALIRI lililopo ndani ya banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere ‘Sabasaba’ jijini Dar es salaam.
Maonesho hayo yanaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Tanzania: Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji”
Tembelea banda hilo ujifunze teknolojia mbalimbali za mifugo zilizoibiliwa na taasisi hiyo.